Jina langu
naitwa halfani ni
mkazi wa bagamoyo tanzania ndipo nilipo zaliwa
katika huu mji
wa zamani .
Nimshiriki wa
spor program kwa
kipindi cha muda
wa miezi mitano nchini
norway kwa kushirikiana na watu wa
jamii ya norway
.
Kwa kupitia
hii program Nilijifuza
mambo mbalimbali katika
hio jamii kama
mifugo kwa ujumla
niliona tofauti sana
hapa tanzania na norway, kwasababu wenzetu utumia mfumo
wa ufugaji wa
kisasa kwa kutumia
mashine katika uzalishaji upande
wa mifugo na
hivyo inawapelekea wafugaji
wengi kushirikiana na
serikali yao katika
uboreshaji wa mifugo
kwa kutumia njia
ya kisasa ni
tofauti sana na
tanzania.
Wafugaji wa
norway wengi utumia
mashine katika ukamuaji
au uzalishaji wa
maziwa na kuyauza
kiwandani ni tofauti
na tanzania kutumia njia
ya zamani katika ukamuaji
na uuzaji wa maziwa mitaani
ambapo inapelekea mfugaji kutoboresha
mifugo yake hapa nchini.
Pia katika
ufugaji wa norway
ni wakisasa zaidi
hasa katika ulishaji
kwa mifugo hutumia
mashine ,ulimaji wa majani
na uvunaji wa
majani wanatumia mashine
na shughuli zote
za mifugo na
shamba utumia zaidi
mashine ambapo ina
mpelekea mtu kutochoka
haraka zaidi ni tofauti na hapa kwetu nchini tanzania
kutokutumia njia za
kisasa katika ufugaji
na kudidimia kilimo
na ufugaji hapa
nchini tanzania.
Pia unakuta
mifugo uwekwa mahali
pazuri kulipo jengewa jengo la
kisasa na kupata huduma
zote humohumo na
kufanya shughuli zote
humohumo ndani ya jengo ni
tofauti na tanzania kutoweka
mifugo mahali pamoja na
kutojengewa sehemu zuri
na kupata huduma zote.
Pia nitofauti
sana hapana tanzania
na norway unakuta
wafugaji wa kinorway
ushirikiana katika shughuli
mbalimbali katika mifugo
kufanya kazi kwa pamoja
na kusaidiana ni tofauti
na watanzania wafugaji
au wakulima kutoshilikiana na
kugombana kila siku
kuzua migogoro ya nchi inapelekea kudidimia
kwa ufugaji na kilimo au kutokua
na maandeleo ya nchi
halfani akiwa katika zizi la ng`ombe la kisasa inchini norway baada ya kumaliza shughuli zote za kazi kwa muda.
halfani akiwa katika shughuli ya kumsafisha ng`ombe chuchu zake kwa ajili ya kukamua maziwa kwa kutumia mashine.
hiii ni nyumba moja wapo ya kisasa kwa ajili ya kuifazia ng`ombe katika mfumo wa kisasa na kupata huduma zote humohumo akiwa katika hii nyumba.
halfani akiwa katika kuweka sawa mashine kwa ajili ya kukamua maziwa ya ng`ombe .
halfani akiwa katika hizi mashine za kukamua maziwa na kuziweka sawa baada ya kukamua maziwa.
halfani akiwa katika shughuli ya kupachika mashine katika chuchu za ng`ombe.
halfani akionganisha mashine kwenye umeme kwa ajili ya kukamua maziwa ya ng`ombe.
halfani akiwa katika mashine kwa ajili ya kijianda na ukamuaji wa maziwa.
hawa ni ng`ombe watoto ambao wakiwa wamehifadhiwa katika zizi la kisasa na kupata mahitaji yote.
halfani akiwa katika shughuli ya kumkata ng`ombe manyoya yake yaliyo kuwa marefu kwa kutumia mashine maalumu.
halfani akiwa katika trekta dogo kwa ajili ya kukusanya majani ya ng`ombe kutoka sehemu moja na kuweka sehemu nyingine.
halfani akiwa katika trekta dogo kwa ajili ya kuchukua majani kuwapelekea ng`ombe.
hawa ni mbuzi wanaofugwa kwa kisasa ambao wamezungurushiwa uzio wa umeme kutozaga mitaani hovyo.
halfani akiwa na familia yake katika mchakato wa kushirikiana kununua ng`ombe kwa ajili ya kuboresha mifugo na uzalishaji wa maziwa.